Nature

Mahakama Kuu Nchini Kenya Wamzuia Ruto Kujenga Kanisa Ikulu

MAHAKAMA Kuu nchini Kenya imetoa agizo la muda ya kuzuia ujenzi wa Kanisa au majengo yoyote yenye mafungamano ya dini ndani ya viunga vya Ikulu ya Nairobi, hatua inayokuja baada ya makundi manne ya kiraia kufungua pingamizi wakidai kuwa ujenzi wa jengo la kidini katika eneo la taasisi ya taifa ni kinyume cha sheria na kanuni za utawala bora.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu, Chacha Mwita ambaye amesema ujenzi huo usitishwe kwa muda hadi pale hukumu ya mwisho itakapotolewa mwezi Novemba 2025 hatua ambayo ni kama ushindi wa muda kwa wanaharakati wa kiraia, huku ukiweka shinikizo jipya kwa serikali kueleza iwapo hatua hiyo inaheshimu misingi ya kikatiba na usawa wa kidini nchini Kenya.

Hivi karibuni Rais wa Nchi hiyo William Ruto alinukuliwa hadharani akisema ameagiza kujengwa kwa Kanisa hilo kwa kutumia fedha zake binafsi, jambo lililozua mijadala mikubwa miongoni mwa wananchi na wadau wa kisheria huku wakosoaji wakisema hata kama fedha ni za binafsi, ujenzi ndani ya lkulu unaweza kufupisha mipaka kati ya dola na dini na hivyo kuibua mgongano wa kikatiba.

Related Posts