Maisha ya Israel Mwenda Yapo Hatarini Yanga Toka Yao Kwasi Kurejea Uwanjani

MBAVU YA KUNESA KULIA:Ukiacha kosa alilofanya kwenye game dhidi ya Dodoma Jiji lililopelekea chuma ya tatu na ya ushindi kwa watu wa zabibu hii ni beki ya mpira haswa yani mazuri ni mengi kuliko makosa anayofanya uwanjani

Kuna kauli me Kwa upande wangu naonaga ni kama yakuwafichia watu makosa yao Kwa kisingizio cha modern football kama wewe ni beki kazi yako ya kwanza ni kuzuia hayo mambo ya sijui kwenda mbele ni ziada timu ikifungwa kupitia njia yako watu hawaangalii tena kwamba we unajua kwenda mbele wanajua we kuzuia Bado kocha anaweza akatengeneza mazingira ya kupata msaada kwenye eneo lako lakini haiondoi uhalisia kua hujui kuzuia vizur

Ila Kwa jeshi mambo yako tofauti yeye anaichapa kama ilivyo Yani kuzuia 90% kwenda mbele 70% uwezo wakupiga mitungi kati watu watie kwenye utosi anao sijui mambo ya kupiga V pasi anao sijui kukokota ngoma balaa tupu kwenye kuzuia haitaji maelezo we mpe game acheze uone ukatili wake
Saizi maisha ya Isra yako mashakani toka imepona hii chuma maana inafanya kila kitu Kwa usahihi mkubwa na ameaminiwa na Pedro na sasa Moalin hii sio bahati mbaya ni uwezo

Jeshi ni fullback ya kwenda na kurudi ilipotokea

Related Posts