Mapingamizi ya Tundu Lissu Kutolewa Majibu Leo

Kesi ya Tundu Lissu Leo
Kesi ya Tundu Lissu Leo

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu leo September 18 2025 amerudishwa tena katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es salaam kwa ajili ya kuendelea na kesi ya uhaini inayomkabili.

Kesi hii inasikilizwa na Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru akisaidiana na Jaji James Karayemaha pamoja na Ferdinand Kiwonde.

Leo hii upande wa Jamhuri unatarajiwa kujibu hoja za mapingamizi ya Lissu ambapo awali Wakili Mkuu wa Serikali Nassoro Katuga aliiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi leo Septemba 18 ili waweze kujibu hoja za Mshitakiwa.

Miongoni mwa hoja za Lissu ambazo leo ataendelea kuziwasilisha Mahakamani ni kwamba katika maelezo ya Mashahidi 30 na maelezo ya Watu 23 kuna makosa hivyo kupitia maelezo hayo anaomba shauri hilo lifutiliwe mbali.

Related Posts