
MARAIS watatu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), Paul Kagame wa Rwanda, Felix Tshiseked wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, wameshindwa kuhudhuria mkutano wa dharura wa 25 wa jumuiya hiyo.
Katibu Mkuu wa EAC, Veronica Nduva, amethibitisha kuwa marais hao wameomba udhuru na wametuma mawaziri wenye dhamana kuwakilisha nchi zao.
Kutohudhuria kwa marais hao kunawafanya marais watano kuja na jina la Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, atakayemrithi Katibu Mkuu wa sasa, Veronica Nduva.
Wanaoshiriki mkutano huo unaoendelea Jijini Arusha, ni Rais wa Kenya, William Ruto ambaye ni Mwenyekiti wa sasa wa EAC, Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni mwenyeji (Tanzania), Rais wa Uganda, Yoweri Museven, Rais wa Burundi, Evarist Ndayishimiye na Rais wa Somalia, Hassan Mahamud.
Licha ya kuja na jina la katibu mkuu mpya, maraisa hao watazindua stakabadhi ya dhamana ya forodha ya jumuiya hiyo
Pia, watazindua mkakati wa maendeleo wa saba wa mpangilio na miradi ya jumuiya hiyo.
Ajenda nyingine za mkutano huo, ni mazungumzo ya kawaida, ambayo Mwenyekiti wa mkutano, ambaye ni Rais wa Kenya William Ruto, atawasilisha ripoti yake kuhusu muhula wake wa Urais na nafasi yake ya Uwenyekiti wa Jumuiya.
“Pia kutakuwa na mabadiliko ya ofisi mbili. Kwanza, Ofisi ya Mwenyekiti. Kama mnavyojua ratiba ambayo ipo na uzoefu uliopo ni kwamba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki huwa anabadilika kila baada ya mwaka mmoja.
“Na kwa sasa kutakuwa na mabadiliko kutoka Kenya, ambayo imekuwa ndio mwenyekiti. Marais wenyewe watazungumza, wataafikiana, halafu watakuwa na Mwenyekiti mpya,” amesema.
Shughuli nyingine itakayofanyika, ni uapisho wa Majaji wa Mahakama ya Haki ya Afrika ya Mashariki (EACJ).
Mkutano huo umehudhuriwa na zaidi ya wajumbe 700 kutoka kila nchi patanishi watashiriki mkutano huo.
