Nature

Marekani Kuchunguza Taarifa ya Raia Wake Kukamatwa Tanzania Kisa Mabomu

Marekani imesema inafuatilia kwa karibu taarifa za kukamatwa kwa mwanajeshi wake ndani ya mipaka ya Tanzania.

Taarifa fupi iliyotolewa kwa Mkuu wa Maudhui wa Crown Media – Salim Kikeke @salim_kikeke na afisa wa ngazi ya juu wa Ubalozi wa Marekani Media imesema:

“Tunafahamu kuwepo na taarifa za raia wa Marekani kukamatwa nchini Tanzania. Tunachukua umuhimu mkubwa jukumu la kusaidia kila raia wa Marekani anayeishi nje ya nchi. Kwa sasa hatuna la zaidi la kulizungumza.”

Umesema ujumbe huo uliotumwa kwa Salim Kikeke @salim_kikeke baada ya kuhoji taarifa hiyo moja kwa moja ubalozini.

Mtu huyo anadaiwa kuwa na uraia pacha wa Marekani na Kenya.

Hivi karibuni vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya Tanzania vilitangaza kukamatwa kwa raia wa Marekani akivuka mpaka kuingia Tanzania akiwa na vilipuzi.

Hii ni mara ya kwanza Marekani kuzungumzia suala hilo.

Related Posts