
Wasaidizi wakuu wa Rais wa Marekani, Donald Trump, wamesema kwamba vituo vya uzalishaji wa umeme na madaraja nchini Iran vinaweza kuzingatiwa kama malengo halali ya Kijeshi.
Kwa mujibu wa ripoti ya Wall Street Journal, Maafisa hao wanasema kuwa kuharibu Miundombinu hii kunaweza kuathiri vibaya programu za Iran za makombora na nyuklia. Hii ni kutokana na hoja kwamba baadhi ya Miundombinu ya kiraia inaweza kuwa muhimu katika kufanikisha miradi ya Kijeshi ya nchi hiyo.
Wasaidizi hao wameeleza kwamba hatua kama hizi, zingeharakisha uwezo wa Marekani kushinikiza Iran kisiasa na kistratejia, huku ikitolewa onyo kuwa mashambulizi yanayohusisha Miundombinu ya kiraia yanaweza kuibua changamoto za Kimataifa.
Ripoti ya Wall Street Journal inaashiria kuwa hoja hizi zinatoa mwongozo kwa sera za usalama wa taifa, huku zikiibua mjadala mkubwa juu ya mipaka kati ya malengo ya kijeshi na Miundombinu ya kiraia.
