
Rais wa Marekani Donald Trump alimwambia Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mwezi Desemba kwamba angeunga mkono mashambulizi ya Israel dhidi ya mpango wa makombora ya masafa marefu ya Iran iwapo Marekani na Iran zisingefikia makubaliano ya nyuklia, kwa mujibu wa ripoti ya CBS News iliyochapishwa Jumapili ikinukuu vyanzo viwili vilivyo karibu na mazungumzo hayo.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa majadiliano kuhusu uwezekano wa shambulio hilo yanaendelea, takriban miezi minane baada ya vita vya siku 12 kati ya Israel na Iran vilivyotokea mwezi Juni mwaka jana. Katika vita hivyo, Marekani ilijiunga na mashambulizi ya Israel dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran
Safari hii, nafasi ya Marekani katika shambulio jipya ingeweza kuhusisha kusaidia ndege za kivita za Israel kujaza mafuta angani au kusaidia kupata ruhusa ya kutumia anga ya nchi jirani ili kupitisha ndege hizo.
