Dar es Salaam 31 Julai 2025: Katika mchakato wa awali kumpata mgombea Ubunge jimbo la Kawe, kupitia Chama cha Mapinduzi, Maria Sebastian ambaye ni msomi na mchapakazi mwenye bidii ya kiwango kikubwa cha ubunifu, uvumbuzi na uwezo wa kupanga na kuongoza jina lake limepenya sambamba na majina mengine kwenye mchujo huo.
Maria Sebastian
Kuhusu elimu yake Maria ana shahada ya uzamili katika utawala wa biashara kwenye mashirika ya umma na stashahada ya juu katika uendeshaji wa benki na fedha kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe na Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (Institute of Finance Management).
Kiuzoefu wa kazi Maria amefanyakazi na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama mchambuzi yakinifu wa biashara ya benki na mifumo ya usalama.
Kwasasa Maria anajitolea katika Chama cha Mapinduzi kama mwanachama mwaminifu na anafanyakazi na jamii katika kuwawezesha wananchi kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Kwa maarifa makubwa aliyoyapata kutokana na utaalamu wake Maria ni kiongozi mpangaji wa mipango, mwelekezaji, mwezeshaji, mjenga timu, mjenga uhusiano, mjenga mikakati, mwenye uwezo wa kuhusiana watu, mpatanishi, mchambuzi yakinifu, msikilizaji mzuri, rahisi kufundishika na tayari kujifunza.
Maria anaonekana kuweza kuleta mabadiliko, kuongeza thamani na kutumia vyema rasilimali na mali zilizopo katika nchi kwa maendeleo ya Jimbo la Kawe.
Maria amekikishukuru Chama cha Mapinduzi kwa kumpitisha kwenye mchujo huo wa awali Maria amesema akipata ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo ataweza kuweka heshima katika kuendeleza yale ambayo viongozi waliopita walianzisha na kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ya uchaguzi 2025- 2030 unafanyika kwa wakati na kugusa maisha ya wananchi.

