Nature

Maskini, Watalii Wawili Wauawa na TEMBO Hifadhi ya Taifa

Watalii wawili wa kike wamefariki dunia baada ya kushambuliwa na tembo jike aliyekuwa na ndama katika Hifadhi ya Taifa ya Luangwa Kusini, mashariki mwa Zambia.

Mkuu wa Polisi wa eneo hilo, Robertson Mweemba, amesema tukio hilo limetokea wakati watalii hao wakiwa kwenye safari ya kutalii wakiwa ndani ya hifadhi hiyo maarufu.

Waliouawa wametambuliwa kuwa ni Easton Janet Taylor (68), raia wa Uingereza, na Alison Jean Taylor (67) kutoka New Zealand. Tembo huyo aliyekuwa akinyonyesha alishambulia kwa ghafla, na licha ya waongoza watalii kujaribu kumzuia kwa kufyatua risasi hewani, juhudi hizo hazikuzaa matunda.

“Wanawake wote wawili walikanyagwa hadi kufa na tembo huyo, na walifariki papo hapo eneo la tukio,” amesema Mweemba.

Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza imethibitisha kifo cha raia wake na kusema inatoa msaada kwa familia ya marehemu huku ikiendelea kushirikiana na mamlaka za Zambia kufuatilia tukio hilo.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *