Matokeo ya SIMBA Vs Yanga, Ngoma Zatoshana Nguvu Kibabe Sana

Simba wamekataa unyonge mbele ya mahasimu wao wa jadi, Young Africans SC (Yanga), baada ya kulazimisha sare ya 0-0 katika mechi kali ya Dabi ya Kariakoo iliyopigwa kwenye dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa na hamasa ya kipekee kutoka kwa mashabiki wa pande zote mbili, ulishuhudia timu zote zikishambuliana kwa zamu, lakini zilikosa umakini wa kumalizia nafasi walizozipata.

Kwa matokeo hayo, Yanga wanaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wakifikisha alama 29 baada ya mechi 11, huku Simba wakibaki nafasi ya tatu, wakiwa pointi tano nyuma ya vinara.

Sare hiyo imeongeza presha katika mbio za ubingwa huku mashabiki wakisubiri kwa hamu mzunguko wa pili wa dabi hiyo yenye historia na ushindani mkubwa nchini.

 

Related Posts