Mbowe Afunguka “Hakuna Kitu Muhimu Kama Uhuru wa Watu Kwenye Nchi Yao”

Mwenyekiti wa zamani wa chama cha Demokrasia na (CHADEMA), Freeman Mbowe, ameitaka Serikali kukiri ukweli na kuwaachia wafungwa wa kisiasa waliopo magerezani ili kuponya majeraha ya watanzania ambao wana maumivu makubwa.

Akizungumza wakati wa salamu fupi za familia katika ibada ya mazishi ya Mzee Mtei, Mbowe amewataka Waziri Mkuu pamoja na viongozi wengine wa serikali kutambua kuwa taifa bado lina maumivu makubwa.

“Nitakuwa mnafiki nisipolisema hili. Maendeleo mnayoniambia serikali inasimamia ni jambo jema, lakini hakuna jambo la maana na la muhimu kuliko uhuru wa watu katika nchi yao,” amesema Mbowe.

Ameongeza kuwa viongozi wa CHADEMA waliopo magerezani wanaendelea kuumiza mioyo ya Watanzania, akisisitiza kuwa magereza yamejaa viongozi wa kisiasa ambao walipaswa kuwa huru, uraiani, wakishiriki na kuona matunda ya nchi yao.
“Njia bora ni kurejesha uhuru wa watu, haki za watu, na serikali ikiri ukweli pale ilipokosea,” amesisitiza Mbowe.

Aidha, amesema kuwa kwa jinsi anavyomfahamu marehemu Mzee Edwin Mtei, alikuwa ni mtu mwenye misimamo thabiti, asiyeyumba na aliyekuwa akitekeleza kwa vitendo ahadi alizoamini.

Related Posts