Nature

MBUNGE Mpina Amvaa Bashe Ununuzi wa Pamba “Hii Kesi Haijaisha”

Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina ameendelea kuikosoa vikali Wizara ya Kilimo kwa kuruhusu mfumo wa mnunuzi mmoja katika ununuzi wa zao la pamba, akidai kuwa mfumo huo unaua ushindani na kushusha bei ya mazao ya wakulima.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Mwandoya, Wilayani Meatu Mkoani Simiyu, Mpina amesema mfumo huo umesababisha bei ya pamba kushuka kutoka Sh. 1,700 hadi Sh. 1,150 kwa kilo, jambo ambalo linawaumiza wakulima wa pamba kote nchini.

“Wizara ya Kilimo hawana pamba, Bodi ya Pamba hawana pamba. Mkataba huu umefungwa na nani? Na kwa nini hauna hata bei iliyoandikwa? Tunafunga mkataba wa kuuza pamba, lazima ieleweke bei ni shilingi ngapi!” alihoji Mpina.

Ameongeza kuwa haoni mantiki ya kuwa na mnunuzi mmoja wa pamba huku mazao mengine kama mtama, mpunga na mifugo yakiuzwa kwa mfumo huru wa ushindani.

“Tunauliza, kwa nini mkataba huu uwe kwenye pamba tu? Kwanini turudi kule tulikotoka?” alisisitiza.

Mpina amesema ataendelea kuishauri na kuisimamia Wizara ya Kilimo ili ibadili mfumo huo usio na tija kwa mkulima.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *