Mchezaji Damaro Amewashika Maungoni Waarabu wa Ahly

Alishindwa Mussa Balla Conte kumwaga jasho pale kwenye kiungo cha Yanga ila kwenye mechi kubwa Mohamed Damaro amewashika maungoni viungo wa Al Ahly leo.

Amepiga pasi 31 zimefika 27 yaani asilimia 87 ya pasi zilikuwa sahihi, amerejesha mpira mara 7 anacheza kiungo wa chini ila ametengeneza nafasi 2 jiulize alipata muda wapi wa kutoka chini kwenda juu.

Ameshuka uvunguni mara 2 na amechukua mpira mara moja dhidi ya Zizo mipira 7 ya juu licha ya ufupi wake ameshinda mara 4 nyie.

Hii ndiyo ilipaswa kuwa replacement ya Khalid Aucho miaka 23 anatosha sana kuwa tegemeo pale shimoni uzuri ni Mmasai wa Kanda ya ziwa Mwanza, Tanzania

Related Posts