Mchezaji Khalid Aucho Avunja Ukimya Baada ya Kusimamishwa Miezi Mitatu

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Khalid Aucho ameandika baada ya klabu yake kutoa taarifa kwa umma kumsimamisha kwa muda wa miezi mitatu.

Aucho amesema kuwa katika kipindi chote cha maisha yake ya soka amekuwa akijiendesha kwa weledi wa hali ya juu, akihakikisha anaziwakilisha klabu zote alizowahi kuzichezea kwa heshima, nidhamu na uwajibikaji.

Amesisitiza kuwa tangu aanze kucheza soka la kulipwa hajawahi kuhusishwa na tukio lolote la utovu wa nidhamu, kwani anatambua kikamilifu wajibu na maadili yanayoambatana na hadhi ya kuwa mchezaji wa kulipwa.

Aidha, amewashukuru mashabiki wake kwa kuendelea kumuunga mkono katika kipindi hiki, akieleza kuwa ana imani hali iliyopo itapita na mambo yatarejea katika mstari wake. Amehitimisha kwa kutoa shukrani za dhati kwa sapoti yao endelevu na kuwaomba waendelee kuwa pamoja naye.

Related Posts