Mchezaji Mo Salah Aonywa Kuhamia Ligi Kuu ya Marekani

Mchezaji Mo Salah Aonywa Kuhamia Ligi Kuu ya Marekani
Mchezaji Mo Salah Aonywa Kuhamia Ligi Kuu ya Marekani

Mkurugenzi wa timu ya Taifa ya Misri Ibrahim Hassan amemtahadharisha Mohamed Salah madai ya kuhamia Ligi Kuu ya soka ya Marekani baada ya kutangaza kuondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu kwa sababu itamfanya fowadi huyo kutofahamika.

Salah (33), bado hajaamua ni wapi atakapohamia baada ya kumaliza kipindi cha mafanikio cha miaka tisa akiwa na Liverpool, ambapo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kamishna wa MLS Don Garber amesema angependa kumuona Salah kwenye Ligi, ingawa haijulikani ikiwa kuna timu za MLS zitajaribu kumsajili.

Hassan alisema Saudi Pro League itakuwa chaguo mwafaka ikiwa Salah atachagua kutosalia Ulaya.

Salah atakosa kambi ya mazoezi inayoendelea ya Misri wakati wanajiandaa kwa Kombe la Dunia huko Amerika Kaskazini.

Misri itamenyana na Uhispania katika mechi ya kirafiki mjini Barcelona Jumanne baada ya kushinda 4-0 dhidi ya Saudi Arabia mjini Jeddah siku ya Ijumaa wiki iliyopita.

Mabingwa hao mara saba wa Afrika wamepangwa Kundi G pamoja na Ubelgiji, New Zealand na Iran katika michuano ya Kombe la Dunia litakayoanza Juni 11 hadi Julai 19.

Related Posts