Nature

Meneja wa Zuchu Afunguka Kilichoharibu Show ya Zuchu Fainali za CHAN

Meneja wa Zuchu, Kim Kayndo, amewatetea wasanii, akisema tatizo si CHAN wala ubora wa wasanii, bali ni miundombinu ya viwanja vya mpira ambavyo havijajengwa kwa ajili ya live music production ya viwango vya dunia. Amesema viwanja hivyo havina acoustic design, hazina line array na delay speakers za kutosha kuondoa mwangwi.

Amefafanua kuwa kwenye maonyesho makubwa ya kimataifa kama Super Bowl halftime show au FIFA Club World Cup performances, mara nyingi playback hutumika kulinda ubora wa matangazo ya televisheni. “Hii inafanywa ili show iwafikie mamilioni ya watazamaji duniani kwa ubora wa hali ya juu,” amesema.

Kayndo ameongeza kuwa msanii anayepiga live kavukavu kwenye viwanja vya mpira analazimika kuwa na utaalamu wa hali ya juu ili kuendesha sauti sambamba na beat bila kupotezwa na delay na mwangwi.

Hivyo, changamoto inayowakumba wasanii wa Tanzania si uzembe wala hujuma, bali mazingira yasiyo rafiki kwa muziki wa kiwango cha juu.

Kwa mtazamo wake, suluhisho pekee ni kuwekeza kwenye sound infrastructure ya viwanja ili matamasha ya muziki Tanzania yaakisi ukubwa wa wasanii wake kwenye jukwaa la kimataifa.

Related Posts