Katika harambee ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inayoendelea leo Agosti 12, katika kumbi za Mlimani City jijini Dar es salaam, Mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed ( GSM) ametoa shilingi Bilioni 10 kama mchango wake kusaidia kampeni za Wagombea wa Urais wa Chama hicho.
Tofauti na mchango huo, Club ya Yanga ambayo anaidhamini nayo imetoa shilingi milioni 100 kuisadia CCM katika Kampeni zake.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye Mgeni rasmi wa harambee hii.
ALSO READ | Edo Kumwembe: Mzize Katoka Kuendesha Bodaboda Hadi Kuuzwa Dola Milion 1


