
MOROCCO; HATUA ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2025 imekamilika na sasa macho yote michezo ya usu fainali itakayofanyika Jumatano Januari 14, 2026.
Kwa mujibu wa ratiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Senegal itacheza na Misri kuanzia saa mbili usiku, kisha saa tano usiku wenyeji Morocco watacheza na Nigeria siku hiyohiyo.
Nigeria imefuzu nusu fainali Januari 10, 2026, baada ya kuifunga Algeria mabao 2-0, wakati Misri yenyewe imeifunga Ivory Coast mabao 3-2. Jana Morocco ilitinga hatua hiyo kwa kuifunga Cameroon mabao 2-0, huku Senegal yenyewe ikiifunga Mali bao 1-0.
