
Siku Moja baada ya mgombea mwenza wa CCM Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kutoa kauli ya ‘kumtaka’ Luhaga Mpina kurejea kwenye chama hicho kutoka ACT Wazalendo aliko hivi sasa, Mpina amesema vigogo wa chama hicho tawala wasahau suala la yeye kurejea kutokana na kile alichodai kuwa chama hicho kimepoteza mwelekeo wake.
Akizungumza na wanahabari waliokaa makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif House, Magomeni jijini Dar es Salaam leo, Jumatano Septemba 03.2025 kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa kesi iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa chama hicho na Luhaga Mpina dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ya kupinga Mpina kuenguliwa kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu (2025), inayoeendeshwa kwa njia ya mtandao chini ya Majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu Dodoma, amesema kwa sasa anaendeleza mapambano ya kupigania maslahi ya Watanzania nje ya chama hicho na amejipanga kikamilifu kuhakikisha mapambano hayo yanafika tamati njema.
From Opera News
Maudhui yaliyoundwa na kutolewa na MediaLab . Opera News ni jukwaa huru hivyo maono na maoni yaliyotolewa humu ni ya mwandishi pekee na hayawakilishi, hayaakisi au hayatoi maoni ya Opera News. Maudhui yoyote/yote yaliyoandikwa na picha zinazoonyeshwa hutolewa na mwanablogu/mwandishi, huonekana humu kama ilivyowasilishwa na mwanablogu/mwandishi na hazijahaririwa na Opera News. Opera News haikubaliani na uchapishaji wa maudhui yoyote ambayo yanakiuka haki (ikiwa ni pamoja na hakimiliki) za wahusika wengine, wala maudhui ambayo yanaweza kuchafua, pamoja na mengine, dini yoyote, kabila, shirika, jinsia, kampuni, au mtu binafsi. Habari za Opera pia haziungi mkono matumizi ya jukwaa letu kwa madhumuni ya kuhimiza/kuidhinisha matamshi ya chuki, ukiukaji wa haki za binadamu na/au matamshi ya asili ya kukashifu. Iwapo maudhui yaliyomo humu yanakiuka haki zako zozote, ikiwa ni pamoja na zile za hakimiliki, na/au kukiuka vipengele vyovyote vilivyotajwa hapo juu, unaombwa kutuarifu mara moja ukitumia barua pepe ifuatayo feedback-opera-news-app@opera.com na/au ripoti makala kwa kutumia sehemu ya kuripoti iliyojumuishwa katika Mfumo wetu.Read more>>

