Mgombea urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, ameapa kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi nchini, akisisitiza kuwa hatapumzika hadi Watanzania wote wanufaike na rasilimali za taifa, na chama hicho kipo makini katika kutatua changamoto za Watanzania.
Akizungumza Agosti 9, 2025 akiwa Zanzibar alipokwenda kutambulishwa kwa Wazanzibar, Mpina amesema: “Hatuna mchezo na taifa letu. Hatutapumzika kulipigania mpaka maendeleo yaliyokusudiwa yafikie wananchi. Watanzania hawawezi kuwa wanyonge kwenye taifa lao, hawawezi kugeuzwa manamba na kikundi kidogo cha watu kinachonyonya fedha za nchi hii.”
Ameongeza kuwa, kufanikisha mabadiliko hayo, ni muhimu Wazanzibar na Watanzania wote kwa ujumla kumpa ushirikiano na kumuunga mkono kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

