Nature

MPINA: Naenda Kuwa Rais wa Kwanza Kutoka Upinzania

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina amesema wananchi wanaomdhamini mwaka huu wanandika historia ya kipekee kwa kumpa nafasi mgombea wa upinzani ambaye atakuwa Rais wa kwanza wa taifa hili kutoka nje ya CCM.

Kauli hiyo ameitoa leo Agosti 18, 2025 akiwa mjini Shinyanga wakati akiomba udhamini wa wananchi ili kukidhi matakwa ya Sheria ya Uchaguzi.

Amesema udhamini wanaoutoa haupaswi kuonekana kama utaratibu wa kisheria pekee, bali kama mchango wa kihistoria wa mabadiliko ya kweli ya uongozi wa nchi.

“Majina yenu yataandikwa kwenye historia kwa sababu mnamdhamini mgombea wa upinzani ambaye atakuwa Rais wa kwanza kutoka upinzani, ambapo safari hii CCM tunaenda kuwang’oa bila huruma,” amesema Mpina.

Related Posts