Staa wa vichekesho Nchini Tanzania Sylvester Mjuni maarufu kama Mpoki, leo katika tukio la msiba la kumuaga Mchekeshaji MC Pilipili, ameonesha kushangazwa na kuhoji ni kwanini hadi sasa hakuna Mtuhumiwa yeyote aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya Mchekeshaji huyo licha ya taarifa ya Polisi kuonesha kuwa kuna Watu walimpigia simu Msaidizi wa MC Pilipili na kumkabidhi MC Pilipili akiwa na hali mbaya baada ya kipigo.
Akiongea wakati wa Ibada ya mazishi ya MC Pilipili Jijini Dodoma leo November 20,2025, Mpoki amesema “Sitaki kulisemea Jeshi la Polisi lakini nimesikiliza ile ripoti Mimi nilitegemea wakati tunazika leo na Watuhumiwa wapo Jela, siliingilii, naheshimu wanalinda usalama wetu na Raia lakini kama kuna Mtu alimpigia simu (Msaidizi wa MC Pilipili) akasema upo wapi tumlete MC Pilipili anzeni na yule mbona kuna Watu wanakamatwa siku moja tu, tuangalie usalama wetu sisi tuko pamoja”
“Lingine kwa upande wa Viongozi kuna kipindi pia MC Pilipili alipitia changamoto (msongo wa mawazo) lakini inaonekana kuna Watu walikaa mbali hawamjasaidia, baadhi ya Viongozi Wasanii wakiwapigia simu pokee simu zao, msiache kupokea tunawasaidia mpaka mnakaa kwenye hivyo viti, tunatumika nyinyi ni Rafiki zetu mfano mzuri Mheshimiwa Mavunde, Mwana FA kila shughuli anakuja lakini kuna Kiongozi akiona simu yako kama kaona msiba hapokei, pokeeni simu kuna wengine tunataka tuwape ushauri tu, asanteni”
Itakumbukwa wakati akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma jana November 19,2025 Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Wiliam Mwanafupa amesema kuwa kabla ya kufariki saa 02:00 mchana, Msaidizi wa MC Pilipili Hassan Ismail alipigiwa simu na Watu asiowafahamu na kuomba wakutane na baada ya muda walifika Watu watatu asiowafahamu wakiwa na MC Pilipili ndani ya gari ndogo nyeupe na walimkabidhi MC Pilipili akiwa na hali mbaya na wao kuondoka.
Millard

