Nature

MPYA! Ndugu wa Humphrey Polepole Ajulikanae Kama Augustino Anasakwa Kuisaidia Polisi Utekaji wa Pole Pole

Jeshi la Polisi limethibitisha kuanza uchunguzi rasmi kuhusu tuhuma zilizotolewa na Bw. Augustino Polepole za kudaiwa kutekwa kwa ndugu yake, Humphrey Polepole. Taarifa hii imetolewa na Jeshi la Polisi yenyewe, na imeanza kutekelezwa tangu jana Oktoba 6, 2025, ambapo jalada la uchunguzi lilifunguliwa siku hiyohiyo.

Katika hatua za awali za uchunguzi, Jeshi la Polisi linafanya jitihada za kukusanya taarifa mbalimbali. Hata hivyo, lengo kuu la sasa ni kumpata Bw. Augustino Polepole mwenyewe. Polisi wanamhitaji Augustino ili aweze kutoa ushirikiano, kutoa maelezo yake kamili, na kutoa uthibitisho wa madai mazito aliyotoa.

Miongoni mwa tuhuma hizo ni pamoja na madai yake kwamba Jeshi la Polisi lilihusika katika tukio hilo la utekaji, taarifa aliyoitoa kupitia mitandao ya kijamii.

Sambamba na kutafuta ushirikiano kutoka kwa Augustino, uchunguzi wa Polisi unalenga pia kuthibitisha hali halisi ya makazi aliyokuwa akiishi Humphrey Polepole. Polisi wanataka kujua kama Humphrey Polepole alikuwa mpangaji ama mkazi wa nyumba anayodaiwa kutekewa, ili kubainisha uhalisi wa eneo hilo katika tukio hilo.

Uchunguzi huu unaendelea na unatarajiwa kutoa majibu ya kina juu ya ukweli wa madai hayo mazito ya utekaji na kuhusishwa kwa Jeshi la Polisi.

Je, Nini maoni yako kufuatia taarifa hii kutokana jeshi la Polisi kufuatia tuhuma ambayo imeshika Vichwa vya watu madai ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba Humphrey Polepole Kutekwa na watu wasio julikana akiwa nyumbani Kwao. Ambapo miongoni mwa mashahidi wa tukio hilo ni ndugu yake Augustino Polepole

Related Posts