Gwiji wa soka la Tanzania, Mrisho Ngasa, amefichua kuwa miongoni mwa wachezaji wanaomvutia zaidi kwa sasa katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara ni winga wa Simba SC, Elie Mpanzu.
Akizungumza juu ya ubora wa wachezaji, Ngasa amesema anakubali kiwango kikubwa cha winga wa Yanga SC, Pacome Zouzou, lakini kwa mtazamo wake binafsi, Mpanzu ndiye anayemvutia zaidi kutokana na ubunifu, kasi na uwezo wake wa kuamua.
Ngasa ameeleza kuwa Pacome ni mchezaji mwenye ubora wa hali ya juu na ana mchango mkubwa kwa Yanga, lakini Mpanzu anamvutia kwa namna anavyocheza.

