Nature
Msando Awaita Maaskofu wa Gwajima, Njooni Tuzungumze

Msando Awaita Maaskofu wa Gwajima, Njooni Tuzungumze

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando amesema atakutana na viongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ili kupata muafaka wa pamoja kutokana na kanisa hilo kufungiwa kwa takribani wiki saba sasa.

Msando amesema hayo leo Julai 20, 2025 baada ya kujiunga kufanya ibada na waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima pamoja na wale wa Kanisa la ABC katika ukumbi wa Tanzanite, ambapo inafanyika semina ya neno la Mungu katika ukumbi huo.

“viongozi wote wa kanisa njooni ofisini tujue hatma ya jambo hili hatuwezi tukakaa hapa kila siku unaamka unajiuliza wananchi wangu wanasali wapi na wanasalije”

Aidha amewahakikishia waumini wa kanisa hilo kuwa watakuwa salama wala hawatakutana na kadhia ya yoyote ikiwemo kukamatwa au kupigwa huku akiahidi atakuwa mtu wa mwisho kutoka kwenye sehemu waliyokuwa wakisali waumini hao.

Pamoja na hayo amesema jambo hilo siyo jepesi lakini anaamini katika mazungumzo watapata muafaka mzuri

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *