Mshambuliaji, Marcus Rashford yupo ukingoni kabisa kuhitimisha utumishi wake wa takribani miaka 20 ndani ya Manchester United baada ya kukamilika kwa nyaraka zote za dili lake la kujiunga na Mabingwa wa Laliga, Barcelona.
Nyota huyo raia wa England amekubali kupunguza mshahara wake kwa asilimia 15 ili kufanikisha kujiunga na Barcelona huku akitarajiwa kulipwa mshahara wa Euro milioni 14 kwa mwaka pamoja na bonasi.
Mashetani hao Wekundu hawatahusika kulipa mshahara as nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa kipindi chote cha mkopo huo huku mkataba huo ukiwa na kipengele cha Barca kumnunua jumla kwa ada ya Euro milioni 30.

