Nature

Mtandao wa Jamii Forums Wapigwa Pini na TCRA, Kwa Madai ya Kuidhalilisha Serikali

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kusitisha kwa muda wa siku tisini (90) leseni ya huduma za maudhui mtandaoni iliyotolewa kwa kampuni ya Vapper Tech Limited, wamiliki wa jukwaa la Jamii Forums, kwa madai ya kuchapisha maudhui ya kupotosha umma, kukashifu na kudhalilisha Serikali pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa ya leo Septemba 06, 2026 iliyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri K. Bakari imeeleza kuwa maudhui hayo yalichapishwa kupitia jukwaa la JamiiForums na akaunti zake za mitandao ya kijamii mnamo Septemba 04, 2025 na kubainisha kwamba yamekiuka Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2020 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2022 na 2025

“TCRA inapenda kuufahamisha umma kuwa, pamoja na kukiuka kanuni, maudhui hayo yanakinzana na utamaduni, mila na desturi za Kitanzania, jambo linaloweza kuathiri umoja, amani na mshikamano wa kitaifa, na pia kuharibu taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” —imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

“Kwa mamlaka iliyopewa chini ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA), Sura 306, TCRA imeamua kuchukua hatua hiyo ya kisheria kwa kusimamisha leseni ya Vapper Tech Limited kuanzia leo, tarehe 06 Septemba 2025, pamoja na kuzuia upatikanaji wa jukwaa la JamiiForums kwa kipindi hicho cha siku 90.” — imesema taarifa hiyo.

Related Posts