Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimewateua Wagombea saba kugombea Ubunge Jimbo la Moshi Vijijini akiwemo Prof, Patrick Ndakidemi, Moris Makoi, Victor Tesha, Deogratius Mushi, Felista Njau, Salim Kikeke na Wiliad Kitali.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla ametangaza majina hayo leo July 29,2025.


