
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limefanikiwa kupata taarifa za kupatikana kwa Mtawa Silianus Korongo (49) ambaye aliripotiwa kutoweka Disemba 1, 2025 kutoka nyumba ya malezi ya watawa wa Shirika la Ndugu Wadogo wa Franciscan (ORDER OF FRIARS MINOR -OFM) iliyopo Kata ya Tungi, mkoani Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 4, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, mtawa huyo amepatikana akiwa salama katika Jiji la Lusaka nchini Zambia akiwa katika nyumba ya malezi ya watawa iitwayo St. Boniventure University.
Taarifa za upatikanaji wa Mtawa huyo nchini Zambia zimethibitishwa na mtawa mlezi wa nyumba hiyo aitwaye Alfigio Tunha.

