Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Abubakari Asenga, ameibua mjadala mzito bungeni baada ya kutoa kauli kali akiwataka Watanzania kuacha tabia ya kumkosoa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na familia yake kwa lugha ya kejeli kwenye mitandao ya kijamii.
Kauli hiyo imekuja wakati ambapo mijadala mikali imekuwa ikiibuka mtandaoni, ikihusisha hata watu wa karibu na Rais, jambo lililoibua hisia tofauti miongoni mwa wananchi.
Akichangia hotuba ya Rais wakati wa ufunguzi wa Bunge la Kumi na Tatu, Asenga alisema wazi kuwa baadhi ya maneno yanayozungumzwa mitandaoni hayalengi kujenga Taifa. Kusoma Zaidi, bonyza hapa.
