
Mtu Mwenye bunduki aina ya Shotgun na dumu la mafuta amepigwa risasi na kuuawa katika eneo la makazi ya Rais wa Marekani Donal Trump Mar-al-Lago wakati wa makabiliano na maafisa wa usalama kutoka United States Secret Service pamoja na Naibu kutoka ofisi ya Sheriff wa Kaunti ya Palm Beach.
Taarifa iliyotolewa na Secret Service imeeleza kuwa mshukiwa alipenya katika eneo ambalo haliruhusiwi kupita hivyo aliamriwa kuweka chini silaha yake(shotgun) lakini inadaiwa aliinyanyua shotgun hiyo katika mkao wa kufyatua risasi.Maafisa walifyatua risasi, na mtu huyo alitangazwa kufariki dunia papo hapo.
Iwapo tukio hili litatambuliwa rasmi kama jaribio la mauaji, litakuwa jaribio la tatu linalojulikana kumlenga Rais Donald Trump katika miaka ya hivi karibuni, jambo linalozua wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa kauli kali za kisiasa kutoka kwa wapinzani wake.
Kihistoria marais wanne wa Marekani waliuawa wakiwa madarakani ambao ni Abraham Lincoln, James A. Garfield, William McKinley na John F. Kennedy.
