
Rais wa Chama cha Wakili Tanzania (TLS), Wakili, Boniface Mwabukusi, amezua gumzo kali kufuatia kauli zake kuhusu ugumu wa kuripoti matukio ya utekaji nyara kwa Rais Samia Suluhu Hassan. Mwabukusi alidai kuwa kuripoti tatizo kama hilo kwa Rais si kazi nyepesi na kwamba mtu anapaswa kuwa makini sana katika namna anavyofikisha taarifa hiyo.
Mwabukusi alielezea jinsi alivyomwambia Rais Samia kuhusu uwepo wa utekaji nyara alisema kwamba kuzungumzia suala la utekaji nyara na Rais si jambo rahisi, ukizingatia uwepo wa viongozi wengine wenye mamlaka kama vile Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Mkuu wa Majeshi, na IGP. Alisema kuwa mtu anapozungumzia suala hilo na Rais, anapaswa kuzingatia hadhi na nafasi ya Rais na kuepuka lugha isiyofaa.
“Hafanyi kazi yoyote. Anafikiri ni rahisi. Rais amekaa hapa, kuna Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, yupo Mkuu wa Majeshi, yupo IGP. Unamweleza Rais kuna tatizo la utekaji. Anafikiri hii ni kazi nyepesi? Vaa viatu vyangu. Ukifika pale utagalagala tu na kusema Rais mitano tena!” Alisema

