Mwanamke Afariki kwa Upasuaji wa Kuongeza Makalio Huko Nigeria, Upasuaji wake Ulileta Shida hii

Simanzi imeghubika Nigeria, kufuatia kifo cha mrembo mwenye umri wa miaka 20, ambaye anasemekana aliangamia akifanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio.

Kulingana na swahiba wa marehemu, Destiny Jojo, alikwenda katika hospitali ya urembo jijini Lagos kwa upasuaji huo na alitarajiwa kuruhusiwa kwenda nyumbani baada ya siku nne. Hata hivyo, alikumbana na matatizo ya kupumua kisha alikimbizwa katika hospitali ya mtalaam ambapo aliaga dunia. Mtu anayedaiwa kuwa shahidi aliyeshiriki tukio hilo kwenye mitandaoni ya kijamii alisema:

“Ilikuwa siku nne baada ya upasuaji wa mrembo huyo, kwa kweli alitakiwa kwenda nyumbani siku hiyo. Lakini asubuhi kama baada ya saa kumi na moja hivi, mwanamke huyo alianza kulalamika kuhusu matatizo ya kupumua. Wauguzi na madaktari walikimbia mara moja na kuanza kumhudumia, wakimpa oksijeni na vitu vingi kisha ikaanza kuonekana kuwa anapata nafuu lakini hawakutaka kuhatarisha, nafikiri kwa sababu ya tukio la zamani. “Waliita sehemu nyingine nje (ICU) iliyokuwa karibu yao na watu wale wakaja na kumbeba. Dada yangu anasisitiza kwamba mwanamke huyo aliondoka hospitalini akiwa hai na kwamba ingawa, alikuwa hapumui vizuri, alikuwa hai na anaongea vizuri sana. Akiulizia kuliko simu yake.”

Related Posts