
Rapa wa Marekani, #FrenchMontana, amepiga hatua kubwa ya kimapenzi baada ya kuripotiwa kuchumbia na #SheikhaMahra, binti wa kifalme wa Dubai. Uhusiano wao ulianza mwishoni mwa 2024 baada ya Sheikha Mahra kutangaza talaka yake.
Sheikha Mahra, aliyezaliwa Februari 26, 1994, ni binti pekee wa Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum na Zoe Grigorakos. Anajulikana kwa juhudi zake za kibinadamu na biashara, ikiwa ni pamoja na kuanzisha chapa ya manukato ya kifahari, Mahra M1, ambayo ilizindua bidhaa ya “Divorce” mwaka 2024.
French Montana, jina halisi Karim Kharbouch, alizaliwa Novemba 9, 1984, Casablanca, Morocco, na baadaye kuhamia New York akiwa na umri wa miaka 13. Alijulikana kwa kazi yake ya muziki kama rapa na albamu yake maarufu Excuse My French (2013) na wimbo wake Unforgettable (2017).
Uhusiano wao umevutia hisia wengi dunian kutokana na mchanganyiko wa kifalme na umaarufu wa kisanii. Wameonekana pamoja kwenye hoteli za kifahari, sherehe za fasheni, na maeneo kama Pont des Arts Paris. Ingawa bado hakuna tarehe rasmi ya harusi, uhusiano huu unatarajiwa kuendelea kuvutia hisia za mashabiki na vyombo vya habari duniani.

