Nature
Anas al-Sharif

Mwandishi Mashuhuri wa Al Jazeera, Anas al-Sharif Auawa Kwa Bomu Gaza

Mwandishi mashuhuri wa Al Jazeera, Anas al-Sharif (28) ambaye amekuwa akiripoti matukio mbalimbali kutoka sehemu nyingi za kaskazini mwa Gaza ameuawa katika shambulio lililolengwa na Israel dhidi ya mahema ya waandishi wa habari katika mji wa Gaza siku ya jana Jumapili, Agosti 10, 2025.

Anas Al-Sharif ameuawa yeye na wenzake wanne (4)
Katika shambulio lililofanywa jana Jumapili jioni dhidi ya hema lililoko nje ya hospitali ya al-Shifa ya Gaza.

Shirika la habari la Al Jazeera limelaani kitendo hicho cha mauaji ya makusudi na kusema kuwa kitendo hicho ni kuminya uhuru wa vyombo vya habari.

Related Posts