
Mwigizaji Elizabeth Michael ( @elizabethmichaelofficial ) amezungumza na waandishi wa habari siku ya leo August 13 ambapo ametangazwa kuwa balozi wa bidhaa za ngozi za Lumina na kueleza kuwa yeye amechagua kutangaza Biashara za watu baada ya Biashara ya nguo aliyofungua miaka mitatu nyuma kumshinda
“Biashara ya Nguo ilinishinda na sio kwa Sababu ya mtaji au uendeshaji, ilinishinda kutokana na muda wangu, ilikuwa inahitaji Muda wako sana, usafiri lakini unajikuta muda mwengine uko shooting so unakuwa Hauwezi kuondoka wiki nzima”
Lulu ameendelea kwa kusema sasa hivi ana focus na kufanya biashara nyingine kama ufugaji na kilimo huku Tayari akiwa anazo Biashara za nyumba ambazo amejenga na kupangisha
“Kwa sasa Biashara yangu nimeamua Kupambana na mabosi nimeona niwe Chawa, niwe ambassador lakini pia nina Biashara nyingine ambazo ni binafsi sana, nataka kujikita Kwenye kulima na kufaga fuga, lakini kitu kingine ambacho napenda ni real estate, kujenga jenga na Tayari Mungu ameshanibariki nyumba ambazo najenga na kupangisha” Lulu Michae
ALSO READ | Harmonize Afunguka Sababu za Kuhairisha Kugombea Ubunge Tandahimba

