Nature

Mwigulu “Kuna Mwanaharakati Katabiri Kuwa Nitakuwa Waziri wa Muda Mfupi zaidi”

Akizungumza leo Novemba 26, 2025, katika Ufunguzi rasmi wa Wiki ya usafiri endelevu ardhini, uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa JNICC jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hata awe Waziri Mkuu kwa wiki moja hataruhusu Tanzania iwe nchi ya Mabwana na Watwana (yenye madaraja)

“Nimemsikia Mwanaharakati mmoja huko ughaibuni anasema huyu ndio atakayekuwa Waziri Mkuu wa muda mfupi zaidi, sawa! Hata niwe Waziri Mkuu kwa wiki moja kwenye wiki hiyo sitaruhusu Watanzania waishi, iwe nchi ya mabwana na Watwana, katika muda huo huo sitaruhusu Watanzania wawe na madaraja. Kwamba kuna sheria imetungwa ya kuwalinda wa daraja la juu na kuwatweza wa daraja la chini. Kwamba akikosea wa daraja la chini anaadhibiwa palepale na wa daraja la juu anapita, analindwa”. Amesema Dkt. Mwigulu

Waziri Mkuu ameongeza kwa kusema kuwa atawasemea wale wa daraja la chini kwa sababu hata akitoka hao ndio atakaoishi nao, hata akifa ndio watakaomzika

Related Posts