Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimewateua Wagombea wanane kugombea Ubunge Jimbo la Mvomero akiwemo Suleiman Ahmed, Stoys Simbachawene, Yusuph Makunja, Jonan Van, Sara Msafiri, Bright Fidelis; Adam Joseph na Prosper Remmy ambapo Burton Mwemba (Mwijaku) ameachwa.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla ametangaza majina hayo leo July 29,2025.

