Paschal Maingu msemaji wa familia ya marehemu Emmanuel Mathias maarufu ‘MC Pilipili’ amesema taarifa aliyoipata kutoka kwa ndugu anasema marehemu amefariki kwa mateso na mwili wake umekutwa na majeraha.
“Mdogo wao wa mwisho aliniambia kapata mateso kabla hajafariki ndio maana mpaka sasa hivi hatuna ratiba yoyote kwaajili ya kumuhifadhi ndugu yetu wakirudi waliokwenda polisi tutajua lakini amechoka” Paschal Maingu – Msemaji wa Familia ya MC PILIPILI

