Nani kuibuka mfungaji bora AFCON 2025?

KUELEKEA mchezo wa fainali wikiendi hii, Januari 18, 2026, vita ya kuiwania tuzo ya mfungaji bora wa msimu huu wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) inaongozwa na staa wa Morocco, Brahim Diaz.

Diaz anayekipiga Real Madrid, ambaye amekuwa wa moto kwenye mashindano hayo, ameshazifumania nyavu mara tano katika mechi sita alizoshuka dimbani.

Straika wa timu ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, Victor Osimhen, na Mohamed Salah wa Misri, wanashika nafasi ya pili, kila mmoja akiwa na mabao manne.

Nyuma yao, kuna kundi la wachezaji watano wenye mabao matatu kila mmoja, ambao ni Ademola Lookman (Nigeria), Amad Diallo (Ivory Coast), Riyad Mahrez (Algeria), Ayoub El Kaabi (Morocco) na Lassine Sinayoko (Mali).

Wakati huo huo, lipo kundi jingine la wachezaji 12, kila mmoja akiwa ameziona nyavu mara mbili. Nyota hao ni Bazoumana Toure (Ivory Coast), Cherif Ndiaye (Senegal) na Christian Kofane (Cameroon).

Wengine ni Elias Achouri (Tunisia), Gael Kakuta (DRC), Geny Catamo (Msumbiji), Ibrahim Maza (Algeria), Iyle Foster (Afrika Kusini) na Nicolas Jackson (Senegal).

Wengine katika orodha hiyo ni Oswin Appollis (Afrika Kusini), Pape Gueye (Senegal), Raphael Onyedika (Nigeria), Akor Adams (Nigeria) na Sadio Mane (Senegal)

Related Posts