
Shirika la Anga la Marekani (NASA), limeanzisha safari mpya ya kihistoria kuelekea mwezini kwa kurusha chombo cha Artemis II, kikiwa na wanaanga wanne.
Safari hiyo ni ya kwanza ya binadamu kuuzunguka mwezi ndani ya zaidi ya nusu karne tangu enzi za programu ya Apollo.
Roketi kubwa ilirushwa kutoka kituo cha Safari za anga cha Kennedy, huku maelfu ya watu wakishuhudia tukio hilo muhimu.
Kikosi hicho kinajumuisha Wamarekani watatu na Mkanada mmoja, na ni safari ya kwanza yenye mchanganyiko mkubwa zaidi wa watu, akiwemo mwanamke.
Wanaanga hao watatumia siku kumi, wakipita karibu na mwezi na kusafiri umbali mkubwa zaidi kuwahi kufikiwa na binadamu kabla ya kurejea duniani.
NASA inasema mafanikio ya safari hii ni hatua muhimu kuelekea lengo la kurejesha binadamu mwezini katika miaka michache ijayo na hatimaye kuanzisha makazi ya kudumu.
Chanzo: DW
