Ndugu wa Diamond Platinumz hawampendi Zuchu


Mara nyingi nashindwa kutoa maoni yangu kwenye mijadala mbalimbali inayoendelea kwa sababu unaweza ukaingia kichwa kichwa ukachangia hoja zako kumbe wenzako walikuwa wanafanya Kiki, ukute mchongo mzima anausimamia Simba mwenyewe na Zuchu anajua hili na lengo lao ni kutrend. Katika nyakati hizi ambazo Wasanii hutegemea kiki na trend ili kukuza muziki na brand zao hakuna linaloshindikana, Meja Kunta amewahi mpaka kuigiza amekufa ili atrend.

Anyways, kama hii issue ya Santos kumbembeleza Ritha arudiane na Diamond ni ya kweli basi Santos amezingua sana na inazidi kuthibitisha namna gani ndugu wa Diamond hawamuelewi Zuchu, mara kadhaa tumekuwa tukisikia hizi stori ila tunapuuzia lakini mianya kama hii inafanya tuamini kuwa Zuchu hapendwi pale ni yeye tu analazimisha penzi. Kama angekuwa anapendwa huyu shemeji yake asingeenda kumdalalia Diamond kwa Mwanamke mwingine, tena Ritha anasema “Diamond si ameshamuoa Zuchu, niacheni na maisha yangu”, kisha Santos anakoleza kuwa “wewe ndiye Sheikh, ulikuwepo wakati anamuoa?”. KIUKWELI HUU NI UNAFIKI NA USALITI WA HALI YA JUU KWA ZUCHU.

Slide ya pili hapo ni Novemba 22, 2025 kwenye Birthday ya Zuchu, Santos alimu-wish kupitia page yake, soma ujumbe ulivyokaa akijifanya anampenda sana kama Shemeji yake kumbe nyuma ya pazia anasuluhisha Simba arudi kwa Ritha. Kiukweli Zuchu awe makini sana, amezungukwa na wanafiki wengi wanaotamani hata leo hii atemwe na Diamond.

By Hopetyga

Related Posts