Mfanyabiashara maarufu na mwanamitandao anayefahamika kwa jina la Niffer, kupitia akaunti yake ya Instagram, ameibua mjadala mkubwa baada ya kushare ujumbe mzito wa kuhamasisha watu kujiamini na kufanya maamuzi magumu bila kuogopa maneno ya watu.
Kupitia ukurasa wake, Niffer aliandika:
“Endelea kushindwa kuchukua maamuzi magumu kwenye maisha yako kisa watu watanionaje!! Kama ukijifunika shuka unalala nao shuka moja basi sawa ❤️
Ila kama unakua mwenyewe, baby, JUST OWN YOUR LIFE.
Nobody really cares about your well being than you.
CHOOSE YOU 📌”
Ujumbe huo umeonekana kugusa wengi, hasa vijana wanaopitia changamoto za kuishi kwa kuogopa hukumu za jamii au presha za watu wanaowazunguka.
Wengi wa wafuasi wake wamempongeza kwa maneno hayo wakidai ni ushauri wa kweli na wa moja kwa moja, unaokumbusha kila mtu kuwa mafanikio na furaha huanza pale unapojipa kipaumbele na kuacha kuishi kwa ajili ya watu wengine.
Kwa tafsiri rahisi, Niffer anaamini kuwa maisha ni yako mwenyewe, hivyo usiruhusu hofu ya “watu watasemaje” ikazuia ndoto na maamuzi yako.
