Nature

Niffer ; Namshukuru Rais Samia Kwa Kuagiza Tupewe Msamaha, Sina Chama Chochote

Mfanyabiashara Jenifer Jovin maarufu ‘Niffer’ amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuagizaa kutolewa kwa msamaha kwa wale wote waliokuwa wanashtakiwa haliyakuwa wamefuata mkumbo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari hii leo Baada ya kuachiwa amesema “Mimi sina la kusema zaidi ya kumshukuru Mheshimiwa Rais, DPP na wote walioshiriki kusaidia sisi kuweza kutolewa”

Mfanyabiashara Jenifer Jovin maarufu ‘Niffer’ amewashukuru Watanzania kwa kuwa karibu naye kwa kipindi chote alichokuwa akishikiliwa na kujitokeza kwa hali na mali kushirikiana na familia yake mpaka alipoachiwa leo Disemba 03, 2025 ambapo amesisitiza kuwa hana chama chochote cha siasa na wala hajihusishi na siasa

Ameyasema hayo leo akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema “sina chama chochote cha siasa na wala sijihusishi na siasa ni Mwananchi wa Tanzania nishukuru mama yangu kwa vyote alivyofanya kwa namna alivyonipigania na Mheshimiwa Rais, niwashukur pia Watanzania ambao waliweza kufika Magereza nawashukuru sana kwa upendo wenu”

Related Posts