Kuna wakati maisha yangu yalikuwa ya aibu na ya kuvunja moyo. Nilikuwa nimechoka kusikia kejeli kutoka kwa majirani na hata ndugu wa karibu ambao waliniona nikihangaika kulipa kodi kila mwezi. Wengine waliniambia wazi kuwa kuishi kwa kupanga ilikuwa ishara ya uvivu na kukosa ndoto.
Nilipokuwa nikishindwa kulipa kodi kwa wakati, nilikuwa nikipigwa kelele na mwenye nyumba kana kwamba mimi si binadamu mwenye heshima. Nilihisi kama dunia yote imenigeukia na hakuna anayejali juhudi zangu.
Nilikuwa nafanya kazi ndogo ya mshahara mdogo sana. Kila nikipata hela zangu, zilikuwa zikielekea moja kwa moja kwenye kodi na gharama ndogo ndogo za maisha. Haikubaki hata senti ya kuweka akiba.
Nilihisi kama nimefungwa kwenye mzunguko wa mateso, na kila mtu aliyenijua aliniona kama mtu asiyeweza kufanikisha maisha yake. Rafiki zangu waliokuwa na nyumba zao walikuwa wakijivunia mali zao, na waliponiona walinikumbusha mara kwa mara kuwa mimi bado nipo nyuma.
Kwa muda mrefu nilivumilia hali hiyo kwa maumivu makubwa. Nilijaribu mikopo mara kadhaa, lakini kila mara nilipojaribu kuomba nilikumbana na vikwazo. Hata mikopo midogo niliyopewa iliniingiza kwenye madeni zaidi. Soma zaidi hapa

