Wakazi wa eneo la Mlimani mjini Morogoro walishuhudia tukio lisilo la kawaida lililomhusisha mwanamke kijana aliyedai kuandamwa na pepo kila alipojaribu kulala. Kila usiku, sauti za ajabu na kelele zisizoelezeka zilianza kumzomea, zikimfanya ashindwe kupata usingizi kwa miezi kadhaa. Wengine walidhani ni ndoto mbaya za kawaida, lakini hali hiyo ilipozidi, ikawa wazi kwamba kulikuwa na kitu kisicho cha kawaida kilichokuwa kikimtokea.
Mwanamke huyo, ambaye kwa sasa anajulikana kwa jina la Janeth M., alikiri kuwa alianza kuona dalili hizo baada ya kifo cha shangazi yake ambaye alikuwa mganga wa kienyeji. Kila alipofumba macho, alihisi kama kuna mtu anampulizia shingoni au anampapasa uso.
Mara nyingine alihisi kama mikono baridi inambeba kutoka kitandani. Hali hiyo ilimnyima amani, ikamfanya awe na woga wa giza na hata kulala. Wazazi wake walijaribu kila njia kutoka kwa wachungaji hadi waganga wa kawaida lakini kila kitu kilionekana kushindikana.
“Nilikuwa naogopa hata jioni ikifika,” anasema Janeth. “Nililala nikiwa nimewaka taa, lakini bado nilihisi uwepo wa kitu kisichokuwa cha kawaida. Nilianza kukonda, nikapoteza hamu ya kula, na hata kazini nilianza kushindwa kufanya vizuri kwa sababu ya usingizi mdogo.” Watu wa karibu walianza kunong’ona kwamba labda kuna pepo wa ukoo aliyekuwa akimfuata” Soma zaidi hapa

