
Kutoka kushoto kwenda kulia: Mwonekano wa setilaiti wa kituo cha kijeshi cha Fuerte Tiuna huko Caracas, kabla ya (Desemba 22, 2025) na baada ya (Januari 3, 2026) operesheni ya kijeshi ya Marekani iliyosababisha kutekwa nyara kwa Rais wa Venezuela Nicolás Maduro. Juu kulia: USS Iwo Jima, meli ya mashambulizi ya Jeshi la Wanamaji la Marekani, iliyopigwa picha wakati wa mazoezi ya NATO mwaka wa 2018; ni ndani ya meli hii ambapo Donald Trump anadai Nicolas Maduro alizuiliwa baada ya kuondolewa kwake na helikopta, kabla ya kuhamishiwa New York. Chini kulia: Picha imechapishwa Januari 3, 2026, kwenye kurasa wa Donald Trump wa Truth Social, ikionyesha kile rais wa Marekani anachowasilisha kama Nicolás Maduro akiwa amefungwa pingu ndani ya meli ya USS Iwo Jima.
Nchini Venezuela, usiku wa kuamkia Januari 3, vikosi vya Marekani vilimteka Rais Nicolas Maduro katika shambulio kubwa lililoitwa “Absolute Resolve,” lililofanywa kwa chini ya saa tano. Uingiliaji huu wa kijeshi na kimahakama, uliodaiwa na Washington, ulielezewa Jumamosi na Mkuu wa Majeshi ya Marekani, Jenerali Dan Caine, wakati wa mkutano na waandishi wa habari pamoja na Rais Donald Trump huko Florida.
Shambulio huo la kijeshi ambalo hapo awali lilipangwa mapema mwezi Desemba, liliahirishwa mara kadhaa huku kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.
Januari 3, hali ya hewa iliboreka vya kutosha,” amesema Jenerali Dan Caine, “ili kuwezesha wanajeshi wa anga wenye uzoefu zaidi duniani kuendesha operesheni hiyo kupitia milima, bahari, na mawingu ya chini.” Saa 4:46 usiku kwa saa za Washington (5:46 alfajiri saa za Ufaransa), Donald Trump alitoa amri ya kuanza operesheni.
Zaidi ya ndege 150 ndege za kivita za F-35 na F-22, ndege za B-1, ndege zisizo na rubani, helikopta, na ndege za upelelezi ziliruka kutoka kwenye kambi ishirini za vikosi vya nchi kavu na majini zinazopatikana kote katika kanda ya Magharibi. Helikopta zilizokuwa zimebeba kikosi cha uchimbaji ziliruka chini ya mita 50 juu ya bahari ili kukwepa rada.
Zilipokaribia pwani ya Venezuela, Marekani ilizima mifumo ya ulinzi wa anga ya nchi hiyo. Caracas ilizama gizani kidogo kufuatia operesheni za kimtandao na kielektroniki zilizofanywa hapo awali. Milipuko ya kwanza ilisikika muda mfupi kabla ya saa 2:00 asubuhi (karibu saa 3:00 saa za Ufaransa). Mashambulizi yaliyolengwa yalipiga vituo vya kijeshi karibu na Caracas, ikiwa ni pamoja na kambi ya anga ya La Carlota.
“Ni mkakati mzuri sana wa kupotosha,” Guillaume Ancel, afisa wa zamani na mwandishi wa blogu “Ne pas souffrir” (Usiudhike), ameiambia RFI. Katika machafuko yaliyofuata, helikopta ziliweza kukaribia alipokuwa, Nicolas Maduro.
Helikopta za kikosi cha kuingilia zilifika mahali ambapo Nicolas Maduro na mkewe walikuwa wamepatikana saa 7:01 usiku (saa za Washington), au saa 8:01 usiku huko Caracas. Vikosi vya Marekani vilishambuliwa na kujibu, na kuharibu ndege moja, lakini bila majeruhi wowote wa Marekani. Kikosi cha kuingilia kati kiliingia katika eneo hilo, kililinda eneo hilo, na kusonga mbele kwa kasi kuelekea lengo lao.
Kulingana na Donald Trump, Nicolas Maduro alijaribu kukimbilia katika chumba salama,” lakini hakufanikiwa. Rais wa Venezuela na mkewe walijisalimisha bila upinzani. “Maduro na mkewe, wote wawili ambao wamefunguliwa mashitaka, walijisalimisha na wanazuiliwa na Wizara ya Sheria,” amebainisha Jenerali Dan Caine.
Baada ya kumkamata Maduro na mke wake wanajeshi wa Marekani huko Caracas waliondoka nae kwa Helikopta chini ya ulinzi wa ndege za kivita na ndege zisizo na rubani zenye silaha. Mapigano kadhaa ya kujilinda yalifanyika wakati wa kuondolewa kwa ndege hizo. Saa 9:29 usiku kwa saa za Washington (4:29 asubuhi saa za Ufaransa), Nicolas Maduro na mkewe walipandishwa katika meli ya Marekani USS Iwo Jima, nje ya pwani ya Venezuela.
Donald Trump alitangaza operesheni hiyo kwenye Jukwa lae la Truth Social saa 10:21 alfajiri (5:21 saa za Ufaransa). Saa chache baadaye, alichapisha picha ya kwanza ya Nicolas Maduro, akiwa amefungwa pingu, amefunikwa macho, na amevaa vipokea sauti vya masikioni vinavyozuia kelele.
Muda mfupi baada ya saa 11:30 jioni kwa saa za Marekani (3:42 asubuhi saa za Ufaransa), alitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Stewart, kaskazini mwa Jiji la New York, kulingana na picha za shirika la habari la AFP zinazomuonyesha akishuka kutoka kwenye ndege akiwa chini ya ulinzi, akiwa amevaa kofia na akiwa amefungwa pingu.
Alipelekwa kwenye ofisi za Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DEA) na kisha hadi Kituo cha Magereza cha Metropolitan Detention Center huko Brooklyn, kulingana na vyombo kadhaa vya habari vya Marekani. Nicolas Maduro na mkewe sasa watakabiliwa na mashtaka katika mahakama za Marekani kwa ugaidi na dawa za kulevya.
Hakuna mwanajeshi wa Marekani aliyeuawa, kulingana na Washington, ingawa majeraha kadhaa yaliripotiwa. Mamlaka ya Venezuela imesema, bila kutoa idadi kamili ya vifo, kwamba raia na wanajeshi wameuawa. Mamlaka huko Caracas imetangaza hali ya hatari nchini kote.
