Nature

Paa la Basi Lang’olewa Likipita Chini ya Daraja

Watu 15 wamejeruhiwa huku mmoja wao akiwa katika hali mbaya baada ya Basi la gorofa walilokuwa wamepanda kugonga daraja na paa lake kung’olewa katika Jiji la Manchester Nchini Uingereza.

Polisi wa Manchester wamesema ajali hiyo imetokea siku ya jumatatu, majira ya saa tisa alasiri kwa saa za Uingereza huku Idara ya huduma za Wagonjwa wa dharura imeeleza kuwa Majeruhi 15 walitibiwa eneo la tukio kisha kupelekwa hospitalini ambapo watu watatu walipata majeraha makubwa huku mmoja wao akiwa katika hali mbaya.

Shirika la Usafirishaji wa Umma (TfGM) Jijini Manchester limesema kuwa Basi hilo lilikuwa na Abiria 100 wakati ajali hiyo imetokea ambapo mmoja wa Mashuhuda wa ajali hiyo amesema hii ni mara yake ya tatu au ya nne kuona Basi likipata ajali kama hiyo katika daraja hilo.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *