Nature

Papa Leo Afunguka “Hakuna Amani Bila Haki”

Papa Leo XIV(Robert Francis Prevost) ametoa wito kwa viongozi wa mataifa duniani kuheshimu maskini na malalamiko waliyonayo huku akisisitiza hakuna amani bila haki.

Kupitia mtandao wa X jana Novemba 16, 2025 Papa huyo aliweka chapisho likisema “Nawasihi Marais na viongozi wa mataifa kuusikiliza ukelele wa maskini.Hakuna amani bila haki.”

Ameeleza kuwa mara kadhaa kilio cha maskini kumekuwa kikinyamazishwa na watawala kupitia kile alichokiita ‘dhana ya ustawi na maendeleo yasiyowajumuisha wote.’

“Maskini wanatukumbusha jambo hili kwa namna mbalimbali, kupitia uhamiaji pamoja na kilio chao, ambacho mara nyingi hunyamazishwa na dhana ya ustawi na maendeleo yasiyowajumuisha wote.” ameandika Papa Leo XIV

Related Posts