Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameshinda kura za maoni za Ubunge wa Arusha Mjini kwa kupata kura 9,056 sawa na asilimia 97.63 ya kura zilizopigwa.
Akitangaza matokeo hayo leo August 04,2025 Msimamizi wa uchaguzi amesema jumla ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo ni 10,186 na waliopiga kura ni 9,276 (91%) ambapo kura zilizoharibika ni 11 na kura halali zilizopigwa ni 9, 265.
Paul Makonda amepata 9,056 (97.63%), Mustafa 83, Gonga 46 , Ali Babu 28, Aminata 26, Mgweno 16 na Kishumbua 10.

